FOR WEDDING PLANNING, FASHION DESIGNING, ART DIRECTION AND STYLING CALL +255 717 514179

Friday

DIAMOND PLATNUMZ AZIDI KUPANDISHA UBORA WA KAZI ZAKE: USAHILI WA VIDEO MODELS 22 Sept 2012


Habari nilizozipata kupitia kwa mkurugenzi wa One touch zinasema,MSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia  kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika kiwango cha kimataifa.
“Jumamosi ijayo tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,” alisema


Akizungumzia kuhusu video hiyo, Mwendapole alisema itarekodi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo msanii huyo analiangalia kwa sasa huku video hiyo ikifanya na kampuni bora kabisa Tanzania.
Kwa upande wake Diamond alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuleta mapinduzi katika sekta ya muziki nchini lakini pia kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana ambao wako mitaani lakini wanapenda muziki.
Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani wiki iliyopita anatarajiwa tena kwenda Marekani kwa ajili ya onyesho moja la muziki.
Msanii huyo alifanya mapinduzi katika medani ya muziki wa bongo baada ya kufanya onyesho lake alilolipa jina la Diamond’s are Forever pale Mlimani City ambapo katika shoo hiyo aliifanya mwenyewe na kiingilio kikiwa sh 50,000 jambo ambalo halijawahi kufanyika katika ulimwengu wa muziki nchini. Haya sasa wale ambao tunasumbuana kila siku mnataka kuuza sura huu ni wakati wako wa kuuza sura pamoja na kulipwa juu sio zile video mnauza bure bure.. kama una mvuto na muonekano mzuri kwanini usipate hili nafasi? lets met next saturday.. Venue nitakujuza soon

1 comment:

  1. KAMA KAWAIDA JEMBE LANGU HALIJAWAHI KUNIANGUSHA...LOVE YOU DIAMOND. KEEP IT UP!!

    ReplyDelete

sema tukusikie